Aliyasema hayo wakati wa mkutano Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Faisal bin Farhan Al Saud katika mji mkuu wa Qatar wa Doha siku ya Alhamisi.
"Tunazingatia uhusiano na nchi za Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, ndugu zetu na kusisitiza haja ya kuweka kando tofauti na kuelekea kwenye maelewano zaidi na mshikamano kwani tunaamini kilichoeneza Uislamu duniani ni urafiki na udugu miongoni mwa Waislamu," Pezeshkian alisema.
Kwingineko katika matamshi yake, Rais wa Iran ameyataja matukio ya kusikitisha katika Ukanda wa Gaza na Lebanon kuwa ni matokeo ya hujuma za utawala ghasibu wa Israel na kusema Waislamu hawapaswi kubaki kughafilika na masaibu yanayowakabili ndugu na dada zao huko Palestina na Lebanon.
Ni kutokana na hitilafu kati ya nchi za Kiislamu ambapo utawala wa Kizayuni unathubutu kufanya jinai na mauaji ya halaiki huko Gaza, alisema.
Pezeshkian pia ameashiria shambulio la kombora la Jeshi la Iran dhidi ya Israel siku ya Jumanne na kusema kwamba ingawa Jamhuri ya Kiislamu haitaki kuzidisha mivutano na migogoro katika eneo, ilifanya operesheni hiyo madhubuti kujibu jinai za utawala wa Tel Aviv.
Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Saudia, kwa upande wake, aliwasilisha salamu kwa Pezeshkian kutoka kwa mwanamfalme wa nchi hiyo ya Kiarabu Mohammad bin Salman na kusisitiza azma ya Riyadh ya kuendeleza uhusiano na Tehran.
Rais wa Iran alifika Doha siku ya Jumatano kwa ziara ya siku mbili kwa mwaliko rasmi wa Amir wa Qatar.
4240387